Michezo

PICHA 4: Yanga wameiondoa Simba kileleni kwa magoli ya Obrey Chirwa

on

Baada ya wekundu wa Msimbazi Simba kushindwa kupata ushindi dhidi ya Azam FC January 28 2017 katika uwanja wa Taifa, leo ilikuwa ni zamu ya watani zao wa jadi Yanga kukabiliana na Mwadui FC katika uwanja wa Taifa.

Mchezo wa Yanga na Mwadui FC ulikuwa ni mgumu kwa timu zote mbili kupata matokeo, kwani Yanga waliingia na dhamira ya kuhakikisha wanaiondoa Simba kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu Tanzania bara ambapo walikaa hapo kwa muda mrefu.

Mwadui FC walikuwa wagumu kuruhusu goli kiasi cha kocha wa Yanga George Lwandamina kufanya mabadiliko yalioisaidia Yanga kwa kumtoa Haruna Niyonzima na kumuingiza mzambia Obrey Chirwa aliyefunga magoli mawili na kuifanya Yanga ipate ushindi wa goli 2-0.

Magoli ya Obrey Chirwa yalifungwa dakika ya 68 na 83 ikiwa ni dakika moja imepita toka aingie akitokea benchi, ushindi huo sasa unaifanya Yanga kuongoza msimamo wa Ligi Kuu na kuishusha Simba kwa tofauti ya point moja, Yanga sasa wametimiza point 46 wakati Simba wao wakisalia na point 45 wakiwa nafasi ya pili katika msimamo wa Ligi Kuu Vodacom.

VIDEO: Yanga vs Azam FC January 7 2017, Full Time 0-4

Soma na hizi

Tupia Comments