fB insta twitter

Maneno ya Dj Choka kwa Mwana FA baada ya kuguswa na hali yake

on

Kutoka Bongoflevani Dj maarufu Bongo Dj Choka amefunguka na kueleza namna staa wa Bongofleva Hamisi Mwinjuma maarufu kama Mwana FA alivyoguswa na hali yake na kumsaidia kumpeleka hospitali.

Kwenye account yake ya Instagram Dj Choka ameandika akieleza namna Mwana FA alivyomsaidia wakati wanatoka Tanga kwenye show ya Sikukuu ya mwaka mpya 2017 ikiwa ni msaada wa kwanza kuupata kutoka kwa staa huyo ambaye alimuwahisha hospitali.

>>>“Shukrani Za DJCHOKA kwa @mwanafaNikiwa sijui kitanitokea nini, baada ya kumaliza show ya HANDENI-TANGA kusherehekea mwaka mpya 2017. Tukiwa tunarudi Dar tarehe 2 January nikiwa kwenye gari mimi na braza Mwanafa ndipo nikaanza kukoo #DAMU mafundo.

“Sikujua ni kitu gani huku tukijiuliza labda ni #NYONGO au kuna tatizo kwenye KOO la hewa. Ndipo ikabidi Mwanafa akimbize gari kuwahi hosp za Dar maana tulikuwa tumeshaingia barabara ya #Msata to #Bagamoyo. 

“Tulifika DAR salama na kuwahi hosp ya Marie Stoper na baadae nikaelekezwa niende Hospital ya Kairuki kwa vipimo zaidi. Kesho yake tarehe 3 nikashauriwa kwenda #Mwananyamala hosp na hapo nilipata vipimo haraka kwa kupima #Mapafu na ndipo nikagundulika nina #KifuaKikuu (#Tuberculosis) na kuanza dozi yake ya miezi 6 kwa Haraka. KifuaKikuuINATIBIKA.” – Dj Choka.

VIDEO: Roma kuhusu kuonekana akifundisha DSM 

Soma na hizi

Tupia Comments