on air with millardayo

VIDEO: Khalid Chokoraa katangaza rasmi kuondoka Mapacha Watatu

on

Mwimbaji wa muziki wa Bendi Khalid Chokoraa ni miongoni mwa wakali wenye majina yao kwenye muziki wa dansi, alipata time ya kufanya Interview na Millard Ayo na akazungumzia taarifa za yeye kutoka bendi ya Mapacha Watatu na kwenda Twanga Pepeta……

‘nimeamua kuondoka bendi ya mapacha watatu, lakini kiheri kabisa, hakuna tatizo wala bifu kikubwa zaidi ni maisha tu, kilichoweza kunisukuma nilijiuliza tunafanya kazi ili tuwe na maisha mazuri ndani ya miaka minane nimefanya nini mbona naona kama siendi vile imetokea mtu ameweka mzigo nikaona tunafanya kazi ili tunatafuta pesa na pesa imekuja’

‘Twanga nilikaa pale miaka mitano nikafanya album nne niliacha viporo vya kazi zangu nyingi sana kwa hiyo nikirudi sitaumiza kichwa sana kwa sababu mashabiki wa muziki wa dansi wanajua nini nilikifanya ndani Twanga Pepeta’;-Khalid Chokoraa

‘Nimepewa ada ya kunirudisha namshukuru Mwenyezi Mungu siwezi kusema ni ndogo au ni nyingi lakini kwa usawa huu wa Magufuli wa kutumbua majipu ni nyingi, kwa kibendi bendi inawezekana katika wanamuziki wa bendi mimi nikawa ni mwanamuziki niliyenunuliwa kwa bei kubwa’:-Khalid Chokoraa

Bonyeza play kwenye hii video hapa chini kupata full interview

ULIIKOSA HII YA CHARZ BABA KUVUNJA MKATABA NA MASHUJAA BAND? UNAWEZA KUANGALIA VIDEO HII HAPA CHINI

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE 

Soma na hizi

Tupia Comments