Utafiti uliofanywa na Wanasayansi kutoka National Research Council umegundua kuwa ulaji wa chipsi au viazi vilivyokaangwa mara mbili au zaidi kwa wiki husababisha vifo vya mapema kwa vijana kwa zaidi ya 70%.
Akielezea utafiti huo Dr. Nicola Veronese amesema ulaji wa viazi hauleti tatizo lolote la kiafya bali vinapokaangwa ndipo hupelekea kiwango kikubwa cha kolestro kunyonywa na mishipa ya damu pindi mtu anapokula hivyo kusababisha ugonjwa wa cardiovascular.
Katika utafiti huu watu 4,440 walihusishwa na walikula chipsi mara tatu kwa wiki kwa muda wa miaka minane ambapo zaidi ya watu 236 walifariki kutokana na ugonjwa wa cardiovascular kuliko magonjwa mengine.
Aidha, wa mujibu wa utafiti huo, imebainika kwamba ukiacha matatizo kama unene kupita kiasi na ugonjwa wa kisukari,ulaji wa chipsi umetajwa kuwa hatari zaidi kwa kusababisha magonjwa yanayopelekea vifo vya haraka.
VIDEO: Wizara ya afya imetaja Mikoa 9 ya Tanzania ibayotakiwa kuchukua hatua kukabiliana na Ebola. Bonyeza play kutazama.