Top Stories

Umoja wa vijana CHADEMA watoa siku mbili kwa Serikali kubadili maamuzi haya …

on

January 29 makao makuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA umefanyika mkutano wa umoja wa baraza la vijana CHADEMA taifa, pamoja na umoja wa CHADEMA wa wanafunzi wa vyuo vikuu CHASO kuzungumza au kufikisha ujumbe kupitia vyombo vya habari kwa kile wanachokiita ni maamuzi yasio sahihi ya serikali.

DSC_0262

Kupitia kwa katibu muhenezi wa CHADEMA taifa Edward Sembeyi wameamua kujadili na kupinga kauli ya serikali kutangaza kufutwa urushwaji wa shughuli za Bunge live, kupitia televisheni ya Taifa TBC. Katibu Sembeyi ametangaza kuwa umoja wa vijana CHADEMA unaungana na chama chao kupinga maamuzi ya serikali yaliotangazwa na waziri wa habari vijana utamaduni sanaa na michezo Nape Nnauye kufutwa kwa urushwaji wa matangazo ya Bunge live.

Umoja wa vijana CHADEMA unapinga maamuzi hayo kwa kile wanachodai kuwa ni sababu dhaifu zilizotolewa kuhusu maamuzi hayo, kwa sababu kwanza serikali inasema inapunguza gharama za urushwa live wa matangazo hayo, lakini wametangaza kuwa mwezi uliopita wamekusanya kodi Trioni 1.3 wakati serikali ya Dk Kikwete ilikuwa inakusanya bilioni  800, kwa takwimu hiyo serikali inazo fedha za kumudu gharama za urushwaji wa matangazo live.

“Majadiliano yanayoendelea katika mitandaoni na kutaka bunge lao liende live wape huru wao na haki ya kuwasikiliza wabunge wao kitu gani wanafanya ndani ya bunge, msimamo wetu sisi vijana wa CHADEMA pamoja na wanafunzi wa vyuo vikuu tunataka Rais atengue kauli ya serikali ya kutokurushwa matangazo ya Bunge live, tunatoa siku hadi jumatatu” >>> Sembeyi

DSC_0265

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye TwitterFBInstagram na YouTUBE wa kubonyezahapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.

Tupia Comments