Top Stories

CHADEMA wamjibu Mbunge Komu “tumbo linampa sababu”

on

Mkurugenzi wa Mawasiliano, Itifaki na Mambo ya Nje wa CHADEMA John Mrema, amesema kuwa Mbunge wa Moshi Vijijini ameamua kutoa kauli hizo kwa kuwa haamini chama kinasimamia nini na kwamba analazimika kubaki ndani ya chama kwa kuwa anasubiri posho zake za Bunge na kiinua mgongo.

“Komu ametangaza kuwa yupo kwenye chama kwa sababu ya kusubiri mafao ya Ubunge na posho za Bunge la Bajeti, kwani amesema kuwa atajiondoa kwenye chama mara baada ya mhula wa Ubunge wake utakapomalizika, akishalipwa mafao yake,  kiufupi tumbo lake ndio linampa sababu ya kubakia ndani ya chama” Mrema.

Aidha Mrema ameongeza kuwa chama hicho kitakaa vikao vyake na kitatoa taarifa rasmi kwa umma juu ya jambo hilo.

PIGO CHADEMA, MBUNGE ATANGAZA KUHAMIA CHAMA KINGINE “IKIWA NITATAKIWA KUGOMBEA NITAHAMIA NCCR”

Soma na hizi

Tupia Comments