Mix

Chadema yasema Mbowe hajulikani alipo yatoa maagizo mazito

on

Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), John Mnyika amekutana na Waandishi wa Habari leo kwenye Makao Makuu ya Chama hicho na kusema mpaka muda huu hawafahamu Mwenyekiti Freeman Mbowe alipo na yupo kwenye hali gani na kusema jambo hilo wanalitafsiri kama utekaji.

Mnyika amesema kwa hatua ya sasa kwasababu Mbowe ni Kiongozi wa Chama Kikuu cha Upinzani na hawajui alipo wanawaomba Wananchi wasaidie kumtafuta.

“Kamati Kuu ya Chama itakutana kesho na kujadili ni maelekezo gani ambayo kama Chama tunapaswa kutoa kwa Wanachama na baada ya kikao hicho tutatoa taarifa kwa Umma, tunawataka Wananchi kuendelea na vuguvugu la kudai Katiba Mpya na wasirudishwe nyuma kwa njia zozote zile”—Mnyika

Tupia Comments