AyoTV

VIDEO: Aliyoyafanya Mzee Ndesamburo CHADEMA enzi za uhai wake

on

May 31, 2017 kiliripotiwa kifo cha Mbunge wa zamani wa Moshi Mjini na Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Kilimanjaro Philemon Ndesamburo na kuthibitishwa na Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe.

Leo June 1, 2017 Viongozi wa CHADEMA wakiongozwa na Katibu Mkuu Vincent Mashinji na mmoja wa waasisi wa chama hicho Victor Kimesera wamekutana na Waandishi wa Habari kueleza mambo kadhaa yaliyofanywa na Ndesamburo.

Victor Kimesera ameeleza baadhi ya mambo hayo yaliyofanywa na mzee Ndesamburokwenye chama hicho, ikiwa ni pamoja na kusaidia ununuzi wa Jengo la Ofisi ya Makao Makuu kwa Tsh. 12m pamoja na kusaidia kupatikana magari mawili yaliyosaidia kuzunguka sehemu tofauti kupata wanachama.

Kwenye VIDEO hii hapa chini kuna mambo yote ambayo ameyafanya mzee Ndesamburo kwa CHADEMA enzi za uhai wake…unaweza kutazama kwa kuonyeza play hapa chini kutazama!!!

VIDEO: Freeman Mbowe kuhusu kifo cha Mzee Ndesamburo, Bonyeza play hapa chini kutazama

Soma na hizi

Tupia Comments