Mix

Kuhusu wanachama wa Chadema waliovuliwa uanachama leo

on

slaaLeo Chadema wametangaza uamuzi yao juu ya wanachama wao Dk. Kitila Mkumbo na Samson Mwigamba kwa kuwavua rasmi  uanachama wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo.

mkumboKamati Kuu ya Chadema ilikutana Januari 3-4, 2014 katika Ukumbi wa Mbezi Garden uliopo jijini Dar es Salaam,Maamuzi hayo ni baada ya kunasa mawasiliano mbalimbali ya Zitto Kabwe na washirika wake akiwemo anayejulikana kwa jina la Chadema Mpya.

mwigambaKatibu Mkuu wa Chadema Dk Willbroad Slaa amezungumza na wanahabari leo na kusema malengo ya waraka wa mabadiliko waliokutwa nao wahusika hayakuwa ya kisiasa tu bali yalikuwa na lengo la kuimaliza chadema na kuwabomoa viongozi wa chama.

Dr slaa pia ameongeza kwa kusema chama kinawatangazia wanachama wote na wapenzi wote kutokushiriki mikutano ama shughuli zozote za kisiasa zitakazoandaliwa na Mbunge wa Kigoma Kaskazini Mh.Zitto Kabwe na washirika wake kwa jina la Chadema.

Source:Gpl

Tupia Comments