Watu 45 wamelazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma kufuatia kula chakula kinachodhaniwa kuwa na sumu wakiwa Msibani, @ayotv_ na millardayo.com imezungumza na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Gilles Muroto na amethibitisha kutokea kwa tukio hilo.
“Watu hao walikuwa Msibani, wakala ugali wa mahindi,maharage na mboga za majani vinavyohisiwa kuwa na sumu, waliolazwa ni 45, Wanawake thelathini, Wanaume wanane na Watoto saba, Madaktari Hospitali ya Mkoa Dodoma, wanafanya juhudi kubwa kuhakikisha wanaokoa maisha yao”-RPC DODOMA
”Tukio limetokea Msibani kuna Mzee mmoja Edward Maduka alifariki, Watu wakakusanyika kula chakula kama ilivyo Jamii, ilikuwa jana saa moja lakini leo saa tano asubuhi Watu wakaanza kutapika na kuharisha, uchunguzi utafanywa kujua kiini cha tatizo na tutatoa taarifa”-RPC DODOMA
“WANAOSEMA BOMBA LA MAFUTA HALIPO NI WAFA MAJI, JIANDAENI KWA AJIRA” RC SHIGELA