Michezo

Uamuzi wa Tanzania bara kuhusu michuano ya Challenge itakayofanyika Ethiopia November 2015

on

Michuano ya timu za taifa za Ukanda wa Afrika Mashariki Kati (CECAFA) ambayo wengi tumeizoea kwa jina la michuano ya Challenge inatarajia kuanza kufanyika November 21 hadi December 6 2015 Ethiopia. Michuano hiyo ambayo mwaka jana haikufanyika kwa kawaida hushirikisha jumla ya nchi 12.

Michuano ya Challenge inatajwa kuwa michuano mikongwe zaidi barani Afrika na mara ya mwisho ilifanyika Kenya na nchi mwenyeji kutwaa ubingwa huo, michuano hii Tanzania ugawanyika kwani Zanzibar hupeleka timu yao ya Zanzibar Heroes lakini Tanzania bara hupeleka kikosi chao cha Kilimanjaro Stars.

DSC_8379

Kupitia Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania TFF limethibitisha October 2 kuwa Kilimanjaro Stars itashiriki michuano hiyo itakayoanza November 21 hadi December 6 Ethiopia. Nchi wanachama wa ukanda wa Afrika Mashariki na kati ambao wanatarajia kushiriki ni Kenya, Uganda, Burundi, Rwanda, Sudan, Sudan Kusini, Tanzania bara, Zanzibar, Ethiopia, Djbout, Somalia na  Eritrea.

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenyeTwitter,FB,Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>>INSTAGRAMTWITTERFBYOUTUBE

Tupia Comments