Jana March 13 2014 kupitia vyombo mbalimbali vya habari ilitoka stori iliyowahusisha Wagombea Ubunge jimbo la Chalinze ambao ni Fabian Leonard Skauki wa CUF na Matheo wa Chadema ambapo C.U.F walisema mgombea wa CHADEMA sio raia wa Tanzania na kwamba kadanganya mambo mengine muhimu.
Leo millardayo.com na AyoTV zimefika tena hadi Bagamoyo Makao makuu ya wilaya Chadema kwa ajili ya kufahamu undani wa madai hayo ya Mgombea wa Cuf ambapo imempata Matheo alieanza kwa kusema >>’kwanza labda niweke sawa zile fomu hakuna sehemu ambayo inasema uambatanishe na vielelezo vya shughuli unayofanya kama yeye alivyosema’
‘Kiuhalisia mimi ni mfanyabiashara wa siku nyingi nafanya biashara na maduka ya nyama, kuhusu kughushi sahihi ya wadhamini hili ni suala ambalo sio la ukweli kwa sababu wakati tunarudisha fomu ilihakikiwa na mkurugenzi ambae ndiye msimamizi wa uchaguzi, sio saini za mkono peke yake zipo za dole gumba na zipo mchanganyiko na tunazo pia zile shahada za wapiga kura, tulifanya uhakiki na shahada zenyewe hivyo mkurugenzi alihakiki na kusema zipo sawa sawa’
‘Kuhusu kusema kuwa mimi sio Mtanzania hilo suala sio la kwangu, nafikiri wanalo uhamiaji au wanalo wenyewe C.U.F mimi ni Mtanzania halali na ninacho kitambulisho cha kupigia kura ambacho nafikiri watanzania wengi ndio wanakitumia’
Kuhusu kusoma na kuandika mgombea huyu amesema ‘fomu nilizijaza mbele ya Mkurugenzi na yeye mwenyewe aliona nafanya kazi hiyo hata katiba yetu inasema kwamba ni kujua kusoma na kuandika, swala la Kiingereza na Kiswahili ni swala la kuchagua lugha unayoiweza na mimi nikachagua Kiswahili kwa sababu ndio lugha ninayoiweza’