Hekaheka za Uchaguzi Mkuu bado zinaendelea na leo September 14, 2020 Chama Cha Democratic Party (DP) kimezindua rasmi kampeni za Urais Kitaifa pamoja na Ilani ya chama hicho katika Viwanja wa Community Centre Manispaa ya Kigoma Ujiji Mkoani Kigoma.
Mgombea Urais wa chama hicho Philipo John Fumbo ameahidi kujenga meli kubwa ya kubeba mizigo na watu itakayofanya safari zake katika Ziwa Tanganyika.