Chama Cha taaluma ya sayansi Kilimo Mazao Tanzania (CROSAT) kinatarajia kufanya mkutano mkuu Mkoani Dodoma kuanzia Disemba 19_20 mwaka huu 2023 Ili Kujadili masuala mbalimbali ya Kilimo Mazao hasa matumizi sahihi ya viuatilifu.
Akizungunza na waandishi wa Habari Katibu mkuu wa Chama hicho Patrick Ngwediagi amesema hivi sasa kumekua na changamoto ya matumizi holela ya viuatilifu bila kufuata ushauri wa Watalam jambo ambalo ni hatari kwa afya ya walaji.
Anasema mkutano huo utalenga kutoa hamasa ya matumizi sahihi ya viuatilifu,mbinu bora za Kilimo pamoja kuishauri serikali masuala mbalimbali ya Kilimo Ili kuinua sekta hiyo.
Ngwediagi anasema licha ya serikali kuwekeza fedha nyingi kwenye miradi ya Kilimo bado wakulima wanahitaji elimu ya Kilimo bora chenye tija Ili kujikomboa kiuchumi.
Katika mkutano huo pia itajadiliwa ajenda ya kupitisha katiba ya chama hicho pamoja semina ya kitaalum Kwa Wataalamu wa Kilimo na wadau wa sekta hiyo Kwa ujumla Disemba 19 .
Kwa upande wake Dkt.Yasinta Nzogale Katibu Msaidizi wa Chama CROSAT amesema pia wanalenga kusaidia wanawake kupitia Kilimo kwa kuwapatia elimu na mbinu bora za Kilimo.
Mgeni rasmi katika mkutano huo akitarajiwa kuwa waziri wa Kilimo Hussein Bashe na washiriki zaidi ya mia mbili kutoa maeneo mbalimbali watakuwepo wakiwemo wakulima ,viongozi wa serikali, wafanyabiashara mbegu na Wataalamu wa sayansi Kilimo Mazao.