Michezo

Chama mali ya Simba mpaka 2022 (+video)

on

Moja ya stori ya kuifahamu leo ni kwamba klabu ya soka ya Simba imesaini miaka miwili na kiungo mshambuliaji  Clatous Chama.

Tangu Jumamosi iliyopita baada ya kumalizika kwa mechi ya Yanga na Simba kwa sare ya bao 1-1, gumzo la kwenye mitandao ya kijamii ilikuwa ni juu ya Yanga kumtangazia Chama kitita cha dola laki mbili (200,000), jambo ambalo limebadili upepo wa mchezo na kujikuta wengi wakibishana juu ya hatima wake.

Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi ya Simba Mohamed Dewji amethibitisha kuwa kiungo huyo amesaini mkataba wa miaka miwili ya kuitumikia Klabu ya Simba.

“Chama hajaenda popote, tumeshasaini nae mkataba hadi 2022, hii ishu ya kwenda Yanga sio ya ukweli, atabaki na Simba mpaka msimu wa 2022 kwahiyo ana msimu nusu na miaka miwili mingine, Mimi kama Mwenyekiti sijawahi kuja kwa Waandishi nikaongea mambo ya longolongo” MO Dewji

GWAJIMA AMUACHA HOI MAGUFULI KWA VICHEKO, MAGUFULI HOI, UMEWAGEUZA CHINI JUU, MBWA ACHA WABWEKE

Soma na hizi

Tupia Comments