Wananchi wa kata ya Mbingu Halmshauri ya Mlimba Wilaya ya Kilombero Mkoani Morogoro wameondokana na kero ya Maji iliyodumu Kwa miaka.mingi baada ya RUWASA Mkoani humo kutelekeza ujenzi wa mradi mkubwa katika eneo hilo
Imeelezwa kuwa mradi wa maji wa Mbingu-Igima unaohudumia watu takriban 6,700 katika vijiji saba vilivyoko kwenye kata za Mbingu na Igima, Jimbo la Mlimba wilayani Kilombero unatarajiwa kukamilika ndani ya wakati, miezi miwili kabla ya muda wa Mkataba ambao ni Septemba 2024.
Hayo yamelezwa leo na Meneja wa Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira (RUWASA) wilaya ya Kilombero, Mhandisi Florence Mlelwa akiwa anatoa taarifa yake ya utekelezaji wa Mradi huo kwenye mapokeo ya Mwenge wa Uhuru uliofika kuona maendeleo ya upatikanaji wa huduma ya Maji Mbingu-Igima.
Mradi huo unajengwa na Mkandarasi Audacia Investment Ltd JV Native Professionals Co:- ambao wameingia Mkataba wa mwaka mmoja na RUWASA Morogoro wa thamani ya Tsh Bil. 2.6 2,674,728,021 kutekeleza Ujenzi wa vituo 105, usambazaji mabomba na ujenzi wa ofisi, unatarajiwa kuwahi kukamilika sababu jitihada zimefanyika na vifaa vyote vya Mradi tayari vimenunuliwa kusubiri kuimarika kwa miundombinu na mvua za masika
Baada ya kupata taarifa hiyo kiongozi wa Mbio za Mwenge wa uhuru Kitaifa 2024 Godfrey Mnzava amepongeza ujenzi wa mradi huo kwa Kutumia mfumo wa tecknologia ya Prepaid Meter za kisasa zinazotumika kwenye vituo vya kulipia kabla ya kupata huduma ambao utapunguza upotevu wa maji ambao ni wakipekee katika mkoa wa Morogoro
Naye mbunge wa Jimbo la Mlimba Godwin Kunambi amemshukuri Rais wa jamhuri ya miungano wa Tanzania kwa kuendelea Kutoa fedha kutekeleza miradi mbalimbali katika Jimbo hilo ikiwemo.miradi ya Maji ,barabara,afya na elimu.
Kwa Upande wao wananchi wa eneo hilo wameipongeza Serikali kupitia RUWASA Kwa kujenga mradi huo kwani utawasaidia kupunguza kutembea umbali mrefu kufuata huduma hiyo ya Maji