Top Stories

‘Chanjo ni salama,Rais umesonga mbele kishujaa’- Waziri wa Afya (Video+)

on

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akishiriki uzinduzi wa chanjo ya Uviko 19 katika viwanja vya Ikulu, Jijini Dar es Salaam.

Unaweza ukatazama live kupitia Ayo TV muda huu Waziri wa Afya Dk. Dorothy Gwajima anazungumza katika hafla hiyo.

‘Mheshimiwa Rais baada ya mapokezi ya  chanjo hujarudi nyuma kwenye kuongoza vita hii dhidi ya Uviko-19 bali umesonga mbele kishujaa na kuhakikisha leo hii asubuhi njema unatangulia mbele kuwaongoza watanzania kwa mfano wa kuchanja mwenyewe kama ishara ya uzinduzi wa utekelezaji’- Waziri wa Afya Dk. Dorothy Gwajima

‘Hivi ni nani ambae angepewa Urais aone kile kitu ni kibaya autangulize mwili wake kwenda kupokea kitu kisichosahihi hii inaonesha kwamba chanjo hizi ni bora na ni salama na zimehakikiwa na vyombo vyote kama ambavyo tumekuwa tukihakiki dawa zote’- Dk. Dorothy Gwajima

‘Hatua hii ni muhimu  katika kuwathibitishia Watanzania kuwa Chanjo ni silaha bora na salama italeta tumaini jipya kwa watanzania katika mapambano dhidi ya Uviko na kuhakikisha kwamba wanaendelea na shughuli za kiuchumi’-Waziri wa Afya Dk. Dorothy Gwajima

Tupia Comments