Katika kuendelea kukuza Sekta ya Utalii nchini Mkuu wawilaya ya Chato Mhandisi Deusdedith Katwale kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa Sekta hiyo tayari wameandaa Maonyesho mbalimbali ya Utalii wilayani humo sambamba na kuleta Fursa kwa Vijana ndani ya chato kupitia vivutio vya utalii pamoja na Michezo.
Akizungumza na Wandishi wa Habari wilayani humo Mhandisi Katwale amesema lengo la Maonyesho hayo ni kutoa Fursa kwa vijana pamoja na Fursa za uwekezaji ndani ya wilaya chato ambapo Mgeni rasmi katika Ufunguzi huo ni Waziri wa Maliasiri na Utalii Bi, Angelina Kairuki ambaye anatarajiwa kufungua Novemba 26.
“Nitumie fursa hii kuushukuru Uongozi wa Simba na Klabu ya Yanga kwa kukubari kushiriki pamoja nasi katika Tamasha chato utalii Festival kwa sababu wao tayari wameshajitoa kuja kushiriki pamoja nasi kuhakikisha kwamba mashabiki wao wanafanya Mechi matata sana ambayo itaenda kuifungua chato kwa namna ya tofauti, ” Mhandisi Katwale.
Mhandisi, Katwale amesema Ufunguzi wa Moanyesho hayo utahudhuliwa na Mpiganaji maarufu wa Ngumi za Kulipwa Karimu Mandonga sambamba na kuambatana na Mechi ya Mashabiki wa simba na yanga pamoja na Mbio za Baiskeli ambapo zitahudhuliwa na wasemaji wa vilabu viwili vya Yanga na Simba.
Kwa upande wake Kamishina Msaidizi wa Uhifadhi kanda ya ya Magharibi TANAPA , Albert Mziray amesema hali ya utalii katika kisiwa cha Rubondo na Hifadhi ya Burigi Chato ambapo wameendelea kushuhudia wageni wakiongezeka kila wakati ambapo hivi karibuni wamepokea wawekezaji wakitaka kuwekeza katika yale Maeneo.
Betha Komba ni Makamu Mwenyekiti wa TTCIA Mkoa wa Geita na Evelyne Bwire ni Katibu TWCC Mkoa wa Geita wamempongeza Mkuu wa wilaya ya Chato pamoja na Mamlka za Hifadhi za Mistu na Wanyama kwa kushirikiana katika kuibua fursa pamoja na uwekezaji ndani ya wilaya hiyo huku wakiahidi kushiriki katika Maonyesho hayo.