AyoTV

Chege kaweka wazi chanzo cha kupishana na Diamond Platnumz kwa ishu ya Mbosso

on

NI Headlines za mkali kutokea Bongo Flevani, Chege ambae time hii amefunguka tetesi zilizodaiwa kuwa yeye na Diamond walipishana kisa Mbosso kusainiwa WCB.

Nilisikia Mbosso kusainiwa WCB wala sikupewa taarifa yoyote kutoka kwa kiongozi wangu wala kutoka kwa kiongozi wa Yamoto Band, sio suala baya,  Je huku umeondoka vizuri ama umeondoka vibaya mbona kimya sina taarifa’– Chege

‘Sikumlaumu Diamond alivyoongea Radioni kwasababu sikuulizwa na kama ningeulizwa basi ningefanunua kauli yangu niliyoitoa na wala sikuwa na sababu kumtakia mabaya Mbosso kwani ndie msanii pekee ambae nilikuwa nampenda Yamoto Band’- Chege

‘Mbosso nimekutana nae Dodoma na nimeongea nae Mengi sana na nikamwambia kauli yangu ilieleweka vibaya na nimemtakia kila la heri WCB kwenye kazi zake na wala sina chuki yoyote’- Chege

CHEGE KAWATUNGIA WIMBO DIAMOND, HARMONIZE NA ALIKIBA WAPATANE KAFUNGUKA HAYA

 

Soma na hizi

Tupia Comments