Michezo

Hawa ndio wachezaji wanne wa Chelsea aliyowataja Mourinho kuwa wanacheza chini ya kiwango …

on

Klabu ya soka ya Chelsea ambayo inashuka dimbani December 14 kucheza mchezo wake wa 16 wa Ligi Kuu Uingereza msimu wa 2015/2016 dhidi ya klabu ya Leicester City. Chelsea inaenda kucheza mchezo huo ikiwa na kumbukumbu ya kupoteza mechi 8 msimu huu katika mechi zake 15 za Ligi ambazo tayari imecheza.

WEST BROMWICH, ENGLAND - AUGUST 23: Referee Mark Clattenburg shows the red card to John Terry of Chelsea during the Barclays Premier League match between West Bromwich Albion and Chelsea at The Hawthorns on August 23, 2015 in West Bromwich, England. (Photo by Michael Regan/Getty Images)

Mara kadhaa kocha wa klabu ya Chelsea Jose Mourinho amekiri kuwa, moja kati ya vitu vinavyochangia kikosi chake kufanya vibaya ni wachezaji kucheza chini ya kiwango, baada ya kuongea maneno hayo mara kadhaa, December 13 Jose Mourinho amewataja wachezaji wake wanne ambao anafikiri hawako katika kiwango chao kama msimu uliyopita.

Chelsea's Branislav Ivanovic, left, and Swansea's Jefferson Montero challenge for the ball during the English Premier League soccer match between Chelsea and Swansea City at Stamford Bridge stadium in London, Saturday, Aug. 8, 2015. (AP Photo/Frank Augstein)

“Kama utaangalia uwezo wa mchezaji mmoja mmoja utaona kuwa Branislav Ivanovic, Gary Cahill, John Terry msimu uliyopita walikuwa na uwezo mzuri sana, lakini huu msimu ni ngumu kusema mchezaji fulani yuko vizuri, uwezo wao karibu wote ni sawa, sioni utofauti wa Cesc Fabregas na wala sioni akiogopa kukaa na mpira wala kufanya makosa” >>>  Jose Mourinho

Cesc-Fabrigas

Klabu ya Chelsea wiki iliyopita ilipoteza mchezo wake wa nane wa Ligi Kuu Uingereza katika dimba lake la nyumbani Stamford Bridge dhidi ya timu iliyopanda daraja msimu huu Bournemouth, licha ya kutwaa Ubingwa msimu uliyopita, Chelsea pamoja na kocha wao Jose Mourinho wapo katika wakati mgumu msimu huu.

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye TwitterFBInstagram na YouTUBE wa kubonyezahapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.

Tupia Comments