Michezo

Kwa matokeo haya ni kweli Chelsea tayari wameivua ubingwa Manchester City?

on

chelseaLigi kuu ya England iliendelea tena usiku wa jana kwa mchezo mmoja kati ya vinara wa ligi hiyo Chelsea na Leicester City kuvaana.

drog

Chelsea ambao wapo kwenye mbio za ubingwa jana waliendeleza ubabe wao na kujihakikishia nafasi nzuri zaidi ya kutwaa kombe hilo baada ya kuilaza Leicester City mabao 3-1.

ter

Ushindi huo umeiwezesha kufikisha pointi 80 wakati waliokuwa mabingwa watetezi, Man City wana pointi 67 na wakishinda mechi zao tatu zilizobaki watafikisha pointi 79.

chels

Sasa Chelsea iliyobakiza mechi nne mkononi, inaendelea kushindana na Arsenal ambayo iwapo itashinda mechi zilizobaki itafikisha pointi 82 hivyo Chelsea inahitaji ushindi wa mechi moja tu kujihakikishia ubingwa.

chee

Chelsea huwenda wakatangaza ubingwa Jumapili ya mwisho wa wiki hii kama watafanikiwa kuwafunga Crystal Palace katika dimba la Stanford Bridge.

Unahitaji chochote ninachokipata kisikupite? jiunge na mimi kwenye Twitter,Facebook na Instagram kwa kubonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.

Tupia Comments