Michezo

Chelsea wamemuamulia Hakim, warudi mezani na Ajax

on

Club ya Chelsea ya England sasa imejipanga kuhakikisha inaboresha safu yake ya kiungo kwa kukamilisha usajili wa Hakim Ziyech kutokea Ajax ya Uholanzi.

Awali inadaiwa kuwa Chelsea walitaka kumsajili Hakim ,26, dirisha dogo la January lakini Ajax walikataa na kusema wako radhi kumuachia mwisho wa msimu.

Chelsea wapo mezani na Ajax kwa sasa wakiwa na ofa nono ya pound milioni 38 zaidi ya Tsh bilioni 100 kwa ajili ya kujihakikishia kuwa mwisho wa msimu nyota huyo anakuwa wao.

Soma na hizi

Tupia Comments