Michezo

Baada ya Pedro Chelsea yamsajili nyota huyu kutoka Brazil

on

Klabu ya Chelsea  ya Uingereza ambayo hadi hivi sasa bado imewekeza nguvu nyingi za kusajili ili kuboresha kikosi chake na kulinda ubingwa wa Ligi Kuu Uingereza ambao wenyewe ndio Mabingwa watetezi wa Kombe hilo, klabu ya Chelsea baada ya kumsajili Pedro August 22 ilithibitisha kumsajili kinda wa Kibrazil.

kenedy

Chelsea kupitia katika account yake ya twitter imethibitisha kumsajili kinda wa Kibrazili Kenedy aliyokuwa anaichezea klabu ya Fluminense ya kwao Brazil. Kenedy ambaye ana umri wa miaka 19 alikuwa ni sehemu ya timu ya Chelsea iliyosafiri na kwenda kuweka kambi Marekani kwa ajili ya maandalizi ya msimu.

Kenedy alicheza mechi moja ya kirafiki kati ya Chelsea dhidi ya FC Barcelona, Washington katika maandalizi ya msimu mpya na August 22 ndio siku uhamisho wake ulipo kamilika.

w213

“Nina furaha kukamilisha uhamisho wangu wa kujiunga na Chelsea ni furaha kwangu kujiunga na mabingwa wa Ligi Kuu Uingereza, natumaini nitakuwa mchezaji muhimu kwa klabu naishukuru Fluminense kuniruhusu kupata hii nafasi”>>>Kenedy

PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia za siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos

Tupia Comments