Michezo

Jose Mourinho kukumbana na adhabu hii baada ya kumbagua kijinsia daktari wa Chelsea..

on

Bado ile ishu ya daktari wa Chelsea na kocha wa timu hiyo Jose Mourinho inazidi kuingia katika headlines licha ya awali kuonekana kama imeisha vile. Baada ya daktari wa Chelsea Eva Carneiro kusimamishwa kutoa huduma katika kikosi cha Chelsea kutokana na Mourinho kumlaumu, kwa sababu aliingia uwanjani kumtibia Eden Hazard wakati wa dakika za lala salama hivyo Mourinho aliona kama  Eva Carneiro alichangia kuchelewesha muda.

Eva Carneiro ambaye anaripotiwa kuondoka rasmi Chelsea anamtuhumu kocha wa klabu hiyo Jose Mourinho kuwa alimfanyia ubaguzi wa kijinsia wakati akitoka uwanjani kumtibia Eden Hazard, stori kutoka 101greatgoals.com na moroccoworldnews.com zinaripoti kuwa ushaidi tayari umekabidhiwa kwa chama cha soka Uingereza FA, uchunguzi ulifanywa kwa kumtumia mtafsiri wa kireno na kubaini kuwa Mourinho alimfanyia ubaguzi wa kijinsia Eva Carneiro.

0E5B88AF00000514-0-image-m-89_1442928966794

Eva Carneiro ambaye toka aingie katika malumbano na kocha huyo wa kireno hajawahi kukaa katika benchi na kuendelea kutoa huduma, Jumanne ya wiki hii alitangaza rasmi kujiuzulu kuendelea kuwa daktari wa Chelsea, kosa alilofanya Mourinho litampelekea kufungiwa mechi tano kwa sababu ya kumtusi Eva Carneiro kwa kutumia lugha ya kireno  “filha de puta” ambapo maana yake ni kuwa binti wa mwanamke muhuni.

Hii ni video ya tukio lenyewe

PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia kuanzia kwenye siasa, muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata,pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>YouTUBE

Tupia Comments