Michezo

Hii ndio hukumu iliyotolewa kwa mashabiki waliomsukuma mtu mweusi nje ya treni Ufaransa..

on

chelsea fannnn

Unawakumbuka wale mashabiki wa Chelsea waliomshusha shabiki mwenzao kwenye treni  ya Paris Metro kisa ana asili ya Afrika?

Mahakana ya Stratford imewapiga marufuku kuhudhuria mechi zote za soka kwa miaka mitano ndani ya Ufaransa.

Richard Barklie, kutoka Carrickfergus, Northern Ireland, Joshua Parsons pamoja na William Simpson wote kutoka Surrey wamepigwa marufuku kuhudhuria mechi baada ya mahakama kuridhika na adhabu hiyo.

hawa

Jaji Gareth Branston alisema kwamba chuki ya kibaguzi iliyooneshwa na mashabiki wa Chelsea katika treni hiyo ya Paris na kiliharibu sifa  soka ya Uingereza.

Ishu hiyo ilitokea wakati mashabiki wa Chelsea walipokuwa katika mji wa Ufaransa wakishabikia mechi ya klabu bingwa Ulaya kati ya Chelsea na Paris Saint Germain July 17 2015.

Baadae ilisambaa video iliyomwonesha raia mmoja wa Ufaransa Souleymane Sylla akisukumwa nje ya treni na mashabiki hao.

Icheki video hapa…

Nitakutumia stori zote ukibonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.

Tupia Comments