Habari za Mastaa

Chege anawazungumziaje mastaa wa bongo wanaotengeneza kiki? kaongea maneno 42

on

Chege Chigunda ni msanii mwingine wa bongofleva kutoka TMK Wanaume family na sasa anayotajwa sana kwenye Radio na TV kutokana na single yake yasweety sweetyaliyomshirikisha Run Town wa Nigeria na kundi la UHURU la Afrika Kusini.

Siku hizi kwenye maisha ya mastaa wengi wa dunia, huwa kuna zile stori wanazitengeneza wenyewe kwa sababu maalum ili kufanya majina yao yaendelee kutajwa kwenye media kila wakati au wakati mwingine wakiwa wanajiandaa kuachia nyimbo au movie mpya ambapo hata Tanzania wapo baadhi wanaoaminika kufanya hivyo yaani ‘kutengeneza kiki’

Kuhusu hii ya kutengeza ‘kiki‘ Chege ambaye alikaa kwenye OnAIR with Millard Ayo amesema yafuatayo >>>Ni mipango unajua kila mtu ana staili yake ya kutoka, kuna mwingine anatoka kwa ukimya hataki stori nyingi… wewe utasikiliza tu kazi yake, ni staili tu na sio kitu kibaya kama inaongeza kitu kwenye game yake, kama inapunguza inabidi kuangalia njia nyingine

Itakuja siku moja Chege atengeneze kiki? majibu yake ni haya >>>staili yangu itabakia hiihii ya kufanya kimyakimya bila kelele nyingi, siwezi kubadilika nikawa mtu wa kutengeneza kiki… sio mimi tu ila TMK hatuna hizo ingawa sio kitu kibaya, inategemea tu na wewe umejitengeneza kwenye mtoko wako

HUJAITAZAMA SWEETY SWEETY BADO? TAZAMA VIDEO YENYEWE HAPA CHINI…

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE

Soma na hizi

Tupia Comments