Top Stories

Chief Kalumuna wa CHADEMA na wenzake waachiwa huru (+picha)

on

Mahakama ya Hakimu Mkazi Bukoba imewaachia huru washtakiwa saba akiwemo aliyekuwa Ngombea wa Ubunge kupitia tiketi ya CHADEMA Jimbo la Bukoba Mjini 2020 Chief Kalumuna ambao walikuwa wanatuhumiwa kwa makosa nane yakiwemo ya kusababisha fujo, kutotii, kusababisha uharibifu wa mali na kusababisha majeraha siku ya kuwaapisha mawakala wa Vyama vya Siasa tarehe 21 mwezi wa 10 mwaka 2020.

Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Bukoba Joseph Lwambano amesema kuwa ushahidi uliotolewa na upande wa mashtaka haukuthibitishwa hivyo inaonyesha washtakiwa hawakuhusika.

Watu mbalimbali wakiwemo wafuasi wa CHADEMA wamejitokeza katika Mahakama hiyo kufuatilia hukumu, na mshtakiwa namba moja Chief Kalumuna alikuwa Diwani kwa awamu mbili na kipindi cha 2015-2020 alikuwa Meya wa Manispaa ya Bukoba.

“BILL GATES NA HELA ZAKE ZOTE KAACHWA, MTAACHANA TU, OBAMA NA MKEWE” WATU WA TWITTER

Soma na hizi

Tupia Comments