AyoTV na millardayo.com imefanya mahojiano na Chifu Athuman Omari Mwariko ambaye alitia nia kugombea katika Jimbo la Moshi Mjini kupitia Chama cha Mapinduzi na katika kura za maoni hakuweza kupata kura za kutosha.
Chifu Mwariko anasema akitokea kuwa Mbunge ataunda Wizara ya Utamaduni ambayo itadili na mambo mbalimbali ya kuwasaidia wananchi ikiwemo kuwapa mshahara kila siku ya Jumamosi wasi na ajaira.
“Wizara ya Utamaduni lazima iwaweke wachawi na warogaji sehemu moja tufanye Research, inaweza ikatokea vita Petrol tukakosa lakini watu wanaweza kuruka na vyombo vingine kwenda DSM au London kwa dakika” Chifu Mwariko