Msemaji wa TikTok amekanusha uvumi kuhusu bilionea Elon Musk kununua programu hiyo maarufu, na kuzitaja kama ni “uongo mtupu”.
ByteDance imepinga marufuku dhidi ya TikTok katika Mahakama Kuu ya Marekani na kulingana na maendeleo ya hivi majuzi, kuna uwezekano kwamba majaji watashikilia marufuku yoyote kwenye jukwaa hilo la video.
Wiki iliyopita, Mahakama ya Juu ilitoa tarehe ya mwisho ya Januari 19 kwa ByteDance kwamba kampuni inapaswa kuiuza TikTok au kupigwa marufuku nchini kwa misingi ya usalama wa kitaifa.
Ripoti ya mtandao wa Bloomberg ilisema Ili kuepusha uwezekano wa kupigwa marufuku nchini Marekani, maafisa wa China wanazingatia mpango wa dharura ambao utahusisha kuiuza TikTok Marekani kwa Elon Musk.
Ikumbukwe kuwa TikTok ilirejea na kuanza kurudisha huduma zake nchini Marekani baada ya Rais Mteule Donald Trump kuruhusu app hiyo kuendelea kufanya kazi Marekani kwa siku 75 huku wakiendelea kutafakari hatua muhimu za kufanya.
TikTok ilikuwa imeacha kufanya kazi kwa watumiaji wa Marekani kutokana na sheria iliyopiga marufuku app hiyo.
Trump amesema atatafuta suluhisho la kuirudisha TikTok, ikiwemo uwezekano wa kushirikiana na kampuni za Marekani.