China imekanusha vikali madai hayo tangu kuanza kwa vita ya Urusi na Ukraine mwaka jana ambapo Rais wa China Xi Jinping amesema mahusiano ya karibu kati ya Urusi na China yanahusu malengo na majukumu mengi ya pamoja na sio kwamba wanaunga mkono Urusi kwenye vita hiyo ambapo China imesisitiza inataka vita hiyo iishe kwa amani.
Katika hatua nyingine Rais Vladmir Putin amemwambia mwenzake wa China Xi Jinping kuwa Urusi iko tayari kuyajadili mapendekezo ya China ya kumaliza mapigano nchini Ukraine, Putin amesema hayo jana mwanzoni mwa mazungumzo kati ya Marais hao nchini Urusi wakati huu ambapo Rais wa China yupo Urusi kwenye ziara yake ya kikazi.
Mkutano wa Marais hao umefanyika wakati China ikitafuta kujiweka kama Nchi isiyoegemea upande wowote katika vita hivyo, Putin na Xi Jinping watakutana tena leo kwa mazungumzo rasmi.