Kando na uungwaji mkono kutoka mataifa ya Magharibi, China pia imeahidi kutoa msaada kwa Morocco.
Shirika la Msalaba Mwekundu la Uchina linasema kuwa litaipa Shirika la Hilali Nyekundu la Morocco $200,000 (£160,000) kwa msaada wa dharura wa kibinadamu, kulingana na vyombo vya habari vya serikali ya China.
Shirika la Msalaba Mwekundu la China lilisema mchango huo utatumika kusaidia Morocco kutekeleza kazi ya uokoaji na majanga, gazeti la China Daily linasema.
Rais Xi Jinping wa China pia ametoa salamu za rambirambi kwa mfalme wa Morocco Mohammed VI.
Waokoaji kutoka China wanafanya kazi katika mji wa kati wa Morocco wa Ben Guerir, kulingana na shirika la utangazaji la CGTN.