Mix

China kufuta hukumu ya kifo?

on

death_penalty

Bunge la China limeazimia kuondoa hukumu ya kifo kwa baadhi ya makosa ambapo rasimu ya mapendekezo ya marekebisho ya katiba tayari imewasilishwa katika bunge la nchi hiyo.

Rasimu ya mabadiliko hayo imewasilishwa kwa ajili ya kusomwa kwa mara ya kwanza katika kikao cha bunge hilo ambacho kinatarajiwa kukaa kwa muda wa miezi 2.

Katika mapendekezo hayo, makosa ambayo yametakiwa kuondolewa adhabu ya hukumu ya kifo ni pamoja na kosa la usafirishaji ama kumiliki silaha na nyuklia kinyume cha sheria, fedha badhia, kujipatia pesa kwa njia ya udanganyifu, kujishughulisha na biashara ya ukahaba, kumzuia askari au mwanajeshi kutimiza wajibu wake, na kuzusha uvumi wa uongo wakati wa kupigana vita.

Iwapo mabadiliko hayo yakifanyika, wale ambao wamekwishahukumiwa adhabu hiyo, watabadilishiwa hukumu na badala yake kukabiliwa na kifungo cha muda mrefu zaidi.

China inatajwa kuwa ni moja ya nchi zinazoongoza kutoa hukumu ya kifo, ambapo taasisi moja ya haki za binadamu ya Dui Hua imesema kwa mwaka jana peke yake China imehukumu kifo kwa takribani watu 2,400 huku kukiwa hakuna takwimu rasmi zilizopatikana mpaka sasa juu ya idadi ya watu wanaonyongwa kila mwaka nchini humo.

Tupia Comments