Duniani

China wako vizuri mtu wangu, hizi ndio bidhaa zao tano wanazoongoza kutengeneza..

on

Bidhaa za China zimekuwa na umaarufu mkubwa sana kwenye nchi za Afrika na Tanzania ikiwemo, lakini sababu kubwa ni kwamba ukiangalia Takwimu za mwaka 2013 na 2014 China imetajwa kuongoza kwa kuwa Nchi yenye Viwanda vingi zaidi Duniani… kwa kuanzia hapo tu kuna uhalali pia China kuongoza kwa kuzalisha baadhi ya bidhaa.

photo1

Hongera nyingi kwao, Ripoti hii hapa nimekutana nayo, kumbe kuna bidhaa ambazo China imetajwa kuongoza kwa kuziingiza bidhaa hizo sokoni sehemu mbalimbali Duniani !! Usishangae pia kuna bidhaa nyingine ambazo ni zaidi ya nusu ya zinazotumika Duniani zimetoka China, japo wengine wanalalamika kwamba bidhaa za Kichina ni FEKI !!

e89a8f5fc4c21763280c10

China inazalisha 70% ya simu zimu zote zinazotengenezwa Duniani, hiyo ni mara kumi zaidi ya wastani wa simu zinazotengenezwa kwenye nchi nyingine Duniani.

IMG-20150915-WA0009

Ripoti zinaonesha China imetengeneza Computer Milioni 286 kwa mwaka 2014, unaambiwa idadi hiyo inakaribia 91% ya Computer zote zilizotengenezwa Duniani mwaka 2014.

131

Wastani wa Idadi ya viatu vinavyozalishwa China kwa mwaka ni Bilioni 13, hiyo ni kama 63% ya viatu vyote vinavyotengenezwa kwa mwaka Duniani.

maxresdefault

China wako vizuri mtu wangu, kwenye Air Conditioners zinazozalishwa Duniani, wao wametengeneza kama 80% hivi ya zote. Kwa hesabu nyingine ni unaambiwa jumla ya AC Bilioni 109 zinatengenezwa China kwa mwaka.

e89a8f5fc4c2176327fd0b

Viwanda vingi viko China, ndio… na hata vya Meli vipo huko pia mtu wangu, kwenye idadi ya Meli zinazotengenezwa kila mwaka Duniani, China wana wastani wa kuzalisha Meli Milioni 766, hiyo inagusa kama 45% ya Meli zote zinazozalishwa Duniani kila mwaka.

PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia kuanzia kwenye siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos

 

 

 

Soma na hizi

Tupia Comments