Duniani

Mchina na Rekodi zake.. ile kufanana na Obama tu, ukimwalika unamlipa Mil. 3 !!

on

Unajua kuna watu wanatengeneza pesa nzuri kwa mtaji mdogo tu, wako wanaoingiza pesa kwa Kipaji cha kuigiza sauti tu za watu maarufu.. lakini yuko Mchina pia ambaye anaingiza Mamilioni kwa kufanana na Rais Barack Obama !!

Ni Raia wa China ambaye anasema kwa mara ya kwanza alijua kwamba anafanana na Rais Obama mwaka 2008 ambapo aliamua kukata nywele zake kwa sababu ya joto >>> “Nilikata nywele zangu kwa sababu ya joto, jamaa yangu mmoja ambaye anapenda sana kufuatilia stori za Obama aliniambia kwamba nimefanana sana na Rais Obama… wakati huo hata sikuwa namfahamu Obama mwenyewe” >>> Hiyo ni nukuu ya Xiao Jiguo, Raia wa China ambaye anaingiza pesa kutokana na kufanana na Rais Obama.

Baada ya hapo jamaa akaanza kumfuatilia Rais Obama kuanzia anavyovaa, anavyoongea na vitu vingine ili kama akimuigiza asikosee… kajitengenezea jina na ikitokea wanampa mwaliko kuhutubia kwa kumuigiza Rais Obama sehemu yoyote anasema huwa analipwa kiasi cha kama Dola 1,500 kwa mwaliko mmoja tu, hiyo inagusa kama Milioni 3.2 hivi za Kitanzania !!

BO Lookalike

Xiao Jiguo akiendelea na majukumu yake.

Sijui Kiingereza ila huwa naongea Kiingereza fake, kwa mtu asiyejua Kiingereza akinisikiliza anaweza akahisi najua lugha hiyo…  wakati mwingine huwa naongea maneno ambayo hata mimi siyaelewi maana yake“- Xiao Jiguo.

Mbali ya hayo madili ambayo jamaa huwa anakutana nayo, iko pia deal ya movie ambayo anaicheza itatoka mwaka 2016… kabla Jiguo hajaupata umaarufu huo alikuwa ni Mlinzi kwa kipindi cha karibia miaka 10 kwenye Kiwanda kikubwa China.

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye TwitterFBInstagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE

Soma na hizi

Tupia Comments