Duniani

Cheki na mgahawa wa kichina, huduma zote unaagiza kwa simu.. hakuna mhudumu !! (+Video)

on

Najua ni mazoea au kawaida kila unapoenda sehemu ya huduma kama mgahawani, hotelini unakutana na wahudumu ambao wanakupokea, wanakukaribisha kwa ukarimu kabisa.. alafu unaanza kuulizwa unahitaji huduma gani ?!

China hayo mambo huyakuti kila sehemu… hiyo kazi yote imeachiwa simu yako aisee !! Mgahawa mmoja uliopewa jina la Renrenxiang Restaurant, uliopo Beijing China hakuna mhudumu kabisa… mteja anaingia hapo na huduma yoyote anayoitaka anaagiza kwa kutumia App iliyopo kwenye smartphone yake.. chochote unachokitaka unaagiza hapo na unaandaliwa !!

Mmiliki wa mgahawa huo Liu Zheng anasema huo ni mwanzo tu, ana mpango wa kufanya mabadiliko ya kuwa na hoteli ya kisasa ambayo haitakuwa na wahudumu kabisa, kuanzia waiter, cashier wala wapishi ambao mteja atakutana nao uso kwa uso… mambo yote kwenye App ya simu yako unajihudumia.

Video na stori yake hii hapa mtu wangu, ucheki na mambo ya Wachina.

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye TwitterFBInstagram na YouTUBE wa kubonyezahapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.

Soma na hizi

Tupia Comments