Habari za Mastaa

Monday Playlist yako iwe na hii mpya kutoka kwa Christina Milian, ‘Like Me’ feat. Snoop Dogg – (Audio).

on

Licha ya kuachana na Lil Wayne, staa wa muziki wa R&B Marekani, Christina Milian anaendelea kuweka headlines na TV Show zake ‘Grandfathered’ na ‘Christina Milian Turned Up’… lakini ukiacha hayo Christina pia yupo tayari kuziweka headlines zake kwenye muziki baada ya ukimya wa miaka karibia 10!

Yes mtu wangu, kama wewe ni shabiki mkubwa wa muziki wa Christina Milian basi ipokee hii, tarehe 4 December 2015 Christina ataidondosha EP yake ‘4U’ yenye nyimbo nne tu ikiwa ni project yake ya kwanza toka alivyoachia Alum yake ya mwisho ‘So Amazin’ mwaka 2006.

waynemilian

Kingine kizuri cha kujua kutoka kwa Christina Milian kwa sasa ni ujio wa single yake ya kwanza kutoka kwenye EP yake, wimbo unaitwa ‘Like Me’ project ambayo feature yake imemgusa (Uncle) Snoop Dogg… EP hiyo imebeba pia single mbili alizofanya na Lil Wayne, Rebel na Do It na licha ya kuachana na rapper huyo msanii huyo alikiri kuwa Lil Wayne amekuwa msaada mkubwa kwa kipindi chote alichokuwa akitengeneza project hiyo.

Kuzisikiliza dakika 3 za single mpya ya Christina Milian na Snoop Dogg bonyeza play hapa chini.

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE kwa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FBYOUTUBE

Soma na hizi

Tupia Comments