Michezo

Baada ya miaka 11 bila taji la EPL, hizi ndio sababu 5 za Arsenal kupewa nafasi ya kutwaa taji hilo msimu wa 2015/2016

on

Headlines za Arsenal kufanya vizuri bado zinagonga vichwa vya habari vya magazeti mengi ya michezo dunini, Arsenal kwa sasa ndio timu inayopewa nafasi ya kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Uingereza msimu wa 2015/2016. Sababu za Arsenal kupewa nafasi ya kutwaa ubingwa sio kwa sababu kaifunga Man City. Hizi ndio sababu tano za Arsenal kupewa nafasi ya kutwaa taji la Ligi Kuu Uingereza msimu wa 2015/2016.

5- Cech na Mesut Ozil kuwa vizuri

Baada ya kuwasili Petr Cech kutoka klabu ya Chelsea alikuwa ana nafasi finyu ya kucheza ila baada ya kupewa nafasi ya kucheza alifanya vizuri na kuimarika langoni, Cech amekuwa umahiri mkubwa wa kuokoa mipira ya kona na faulo, pamoja na kiungo wao Mesut Ozil kuwa mahiri katika kuhakikisha anapiga pasi za magoli.

Cech-ball

4- Kujiamini

Arsenal ndio timu pekee katika timu zilizopo nafasi sita za juu inaonekana kujiamini zaidi kwa kila kona, hata ukiangalia uwezo waliouonesha wachezaji wa Arsenal katika mchezo wa Jumatatu dhidi ya Man City unajua kabisa wanahitaji kushinda taji, kimeonekana sasa hivi baada ya Arsenal kuondokewa na mastaa wake miaka kadhaa nyuma.

Walcot-goal

3- Uwepo wa wachezaji nyota

Kwa mara ya kwanza toka ameondoka Thierry Henry, Arsenal ndio imeonekana kusajili wachezaji nyota kadha kutoka timu kubwa, kitu ambacho kimeanza kuonesha dalili za Arsenal kuwa na nia ya dhati, tofauti na siku za karibu walivyokuwa wanasajili wachezaji wachanga. Kwa miaka ya karibuni Arsenal imewasajili wachezaji nyota kama Ozil kutoka Real Madrid, Sanchez kutoka FC Barcelona.

Sanchez15

2- Kukaa miaka 11 bila kutwaa taji la Ligi Kuu Uingereza

Arsenal haijatwaa taji la Ligi Kuu Uingereza toka mwaka 2004, hivyo kwa sasa wachezaji na mashabiki wasingependa kuona hali hiyo ikiendelea kujitokeza, hususani kwa klabu kama ya Arsenal ambayo ni moja kati klabu maarufu na zenye mashabiki wengi duniani.

Henry-LEAGUE

1- Karibia kila timu kubwa Uingereza haiko katika hali nzuri

Arsenal wana bahati msimu huu kwani karibia kila timu ambazo huwa zinapewa nafasi ya kutwaa ubingwa haziko vizuri, hata Bingwa mtetezi wa taji hilo klabu ya Chelsea haiko vizuri kwani hadi sasa ipo nafasi ya 15 ikiwa imepoteza jumla ya michezo 9, ina point 18 yaani tofauti ya point 20 dhidi ya Leicester City inayoongoza Ligi.

Chelsea-sad

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye TwitterFBInstagram na YouTUBE wa kubonyezahapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.

Tupia Comments