Mix

Rais Jakaya Kikwete ametangaza mabadiliko haya ya Mabalozi…

By

on

jkJioni ya Aug 11 Rais Jakaya Kikwete ametangaza mabadiliko ya Mabalozi kadhaa pamoja na Mkurugenzi wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) Mabadiliko hayo yamenifikia pia mtu wangu na barua hiyo imeandikwa hivi.

Kwenye uteuzi huo, Joseph B. Masikitiko anakuwa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS). Kabla ya uteuzi huo Masikitiko alikuwa Kaimu Mtendaji Mkuu wa Shirika hilo (TBS).

Upande wa Mabalozi walioteuliwa list yao ni hii hapa.

(i) Lt. Gen. Charles L. Makakala, ameteuliwa kuwa Balozi wa Tanzania Zimbabwe… Kabla ya uteuzi huo, alikuwa Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Ulinzi (National Defence College).

(ii) Balozi Wilson Masilingi aliyekuwa Balozi wa Tanzania Uholanzi, amehamishwa kwenda kuwa Balozi wa Tanzania Marekani kujaza nafasi iliyoachwa wazi na Balozi Liberata Mulamula aliyeteuliwa hivi karibuni kuwa Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Nje ya Nchi na Ushirikiano wa Kimataifa. Atakuwa pia anaiwakilisha Tanzania Mexico.

Wilson Masilingi

Balozi Wilson Masilingi

(iii)Balozi Irene Kasyanju aliyekuwa Mkurugenzi wa Idara ya Sheria, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, ameteuliwa kuwa Balozi wa Tanzania Uholanzi kushika nafasi inayoachwa wazi na Balozi Wilson Masilingi.

 Balozi Irene Kasyanju

Balozi Irene Kasyanju

Taarifa imetolewa Jumanne, Agosti 11, 2015 na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue Dar es Salaam na Uteuzi na uhamisho huu unaanzia tarehe 07 August 2015.

PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia za siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos

Tupia Comments