Duniani

China wameamua mabadiliko kuanzia January 2016 kuhusu idadi ya watoto kwa wanandoa..

on

Tunajua na imekuwa ikifahamika kwamba kwa kipindi kirefu China wamekuwa na utaratibu wa kila wanandoa au wapenzi kuruhusiwa kuwa na mtoto mmoja tu… japo China wana Sheria hiyo bado ni nchi inayoongoza kwa kuwa na watu wengi zaidi duniani !!

Kwa sasa China ina jumla ya watu Bilioni 1.35 ikifatiwa na India yenye watu bilioni 1.25… Kumekuwa na stori nyingi zikihusisha na mipango ya China kubadili Sheria ya mtoto mmoja kwa kila wanandoa na wapenzi, kilichonifikia ni kwamba tayari imepitishwa kwamba kuanzia January 1 2016 wanandoa na wapenzi wataruhusiwa kuwa na watoto wawili.

Msisitizo umetolewa na Serikali China kwamba uamuzi huu umetoka kwa wakati sahihi kwa sababu ya kuhakikisha kunakuwa na usawa kwenye umri watu wao wa China ambapo kwa sasa wazee na watu wazima ni wengi kuliko watoto na vijana.

Kwa hesabu zilizopigwa ni kwamba kwa mabadiliko hayo, mpaka mwaka 2050 China itakuwa na jumla ya watu bilioni 1.46… Stori iko pia kwenye hii video.

https://www.youtube.com/watch?v=KRuwrz4LwQs

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE

Soma na hizi

Tupia Comments