Chama cha soka cha Ghana (GFA) kimemtangaza Kocha wa zamani wa Brighton na Newcastle United za England Chris Hughton kuwa Kocha wao Mkuu wa Timu ya Taifa.
Mtihani wa kwanza wa Chris Hughton kama Kocha wa Ghana ni mechi za kuwania kufuzu kucheza AFCON 2023 dhidi ya Angola.
Chris Hughton alikuwa mshauri wa Ghana katika michuano ya Kombe la Dunia na sasa anaingia kuchukua nafasi ya Otto Addo ambaye ameondoka baada ya Kombe la Dunia Qatar.