Habari za Mastaa

Nyumbani kwa Chris Brown kuna nini?!.. Nyingine ya mwanamke kuvamia nyumba yake imenifikia!

on

Miezi kadhaa iliyopita, Chris Brown aliziandika headlines baada ya taarifa kusambaa kuwa kuna mwanamke alivamia nyumba yake na kujikaribisha mpka ndani pamoja na kuchora kuta za nyumba za staa huyo na maandishi yaliyosema ‘I Love You Chris’… hiyo ilikuwa miezi saba iliyopita, kuna nyingine mpya inayofanana na hiyo pia!

BEVERLY HILLS, CA - FEBRUARY 07: Recording artist Chris Brown attends the Pre-GRAMMY Gala and Salute To Industry Icons honoring Martin Bandier at The Beverly Hilton Hotel on February 7, 2015 in Beverly Hills, California. (Photo by Jason Merritt/Getty Images)

Siku ya jumanne tarehe 22 December 2015, Chris Brown alipata ugeni mwingine unaofanana na huo sema time hii kwa mujibu wa mtandao wa TMZ mwanamke aliyevamia nyumba ya Chris alisubiri mpaka staa huyo atoke ili aweze kupata chance ya kuingia nyumbani kwake… Walinzi wakauomba aondoke lakini dada huyo akagoma kabisa na kutaka kubaki!

NEW YORK, NY - FEBRUARY 16: Chris Brown performs onstage during the "Between The Sheets" tour at Barclays Center of Brooklyn on February 16, 2015 in New York City. (Photo by Theo Wargo/Getty Images for Live Nation)

Mtandao wa TMZ umeripoti kuwa baada ya polisi kuja na Chris Brown kurudi nyumbani baada ya kupewa taarifa ya kilichotokea, dada huyo alikamatwa na kutolewa ndani ya nyumba ya staa huyo kwa nguvu na muda wote huo Chris alikuwa ndani na kugoma kutoka.

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>>  INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE


Soma na hizi

Tupia Comments