fB insta twitter

Unafahamu ‘kibarua kipya’ alichopewa Chris Brown na Mahakama? Soma hapa mtu wangu.

on

Chris_brown_court_APStori mpya ninayokuletea mtu wangu wa nguvu inamhusu mwanamuziki Chris Brown, huenda hujapata nafasi ya kukutana na stori zake hivi karibuni, nakuletea hii ambayo ni latest zaidi kuhusiana na jamaa huyo.

Ripoti ya nguvu niliyoipata TMZ kuhusiana na Chris Brown inasema jamaa kapewa dili la nguvu na mahakama litakayomuweka busy mpaka Januari Mwaka 2015, kutokana na kibarua chenyewe kuwa na ratiba tight ya aina yake.

Chris Brown amepewa ‘dili’ la kufanya kazi za kijamii kwa masaa nane kila siku, na kwa mujibu wa ratiba aliyopewa na mahakama anatakiwa afanye kazi hizo kwa siku 4 kila wiki, ikimaanisha ni siku 1 tu ndani ya wiki kuanzia Jumatatu mpaka Ijumaa ambazo ‘atadeal’ na mambo yake mengine.

Utetezi wa daktari wake huenda usimuokoe Chris kwenye ‘kitanzi cha ajira’ hiyo kutokana na matukio kadha aliyoyafanya kipindi akiwa chini ya uangalizi wa mahakama juu ya mwenendo wake baada ya kukabiliwa na kesi ya kumtwanga makonde mpenzi wake wa zamani, Rihanna.

Chris Brown

Ni halali yako kupata kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>> twitter Insta Facebook

Tupia Comments