Akiwa kwenye mbio za kuitangaza Album yake mpya, ROYALTY msanii wa muziki wa R&B kutoka Marekani, Chris Brown alichukuwa time na kutembelea studio ya HOT 97 kwa ajili ya interview na kipindi cha Ebro in The Morning siku ya jumanne asubuhi.
Kwenye interview yake, Chris aligusia vitu vingi ikiwa maisha yake binafsi, majukumu ya kuwa baba na mipango yake ya Christmas na kama ilivyo kwa wasanii wengi wa muziki Chris Brown hakupenda kabisa kugusia topic nzima ya siasa lakini alichoweza kugusia Chris ni issue ya yeye kusemwa kutokana na watu anaokaa nao karibu pamoja na mpenzi wake wa zamani Karrueche Tran.
Kuhusu company yake ya marafiki, Chris Brown alisema: >>> “Nimezaliwa nimekuta hii ndio jamii ya watu inayonizunguka.. sisemei vikundi vya uhalifu ila nimezaliwa na kujikuta nimezungukwa na umasikini, nimezaliwa nimejikuta nimezungukwa na mitaa mibovu. Na watu ninaoweza kuelewana nao ni watu waliokua kwenye mazingira kama yangu… mazingira kama hayo“. <<< Chris Brown.
Kuhusiana na mpenzi wake wa zamani, Chris Brown amesema hana mawasiliano yoyote yale naye ila anamtakia baraka na mafanikio yote maishani… >>> “Sina mawasiliano yoyote yale na Karrueche, lakini namtakia mafanikio na baraka zote maishani na kwenye kazi zake…” <<< Chris Brown.
Swali la Chris lilitokana na interview ya awali aliyowahi kufanya Karrueche Tran ambapo alipoulizwa kuhusu kuwa na mpenzi, model na actress huyo alijibu kwa kusema… >>> “Sipo tayari kiakili na kisaikolojia kuwa na mpenzi kwa sasa, na siwashangai watu wanaogopa kujihusisha kimapenzi na mimi kwa sababu ya drama za Chris, kwani nilijitoa sana kwa Chris na mpaka sasa bado naumizwa na maamuzi yake ya kuzaa na mwanamke mwengine...” <<< Karrueche Tran.
Alipoulizwa kwanini aliamua kumshambulia Tyson Beckford kwenye mitandao ya kijamii baada ya ‘kuhisi’ ana mahusiano na Karrueche, Chris alikuwa muwazi na kusema…. >>> “Nilikuwa tu na wivu na nilikuwa sijiamini… nilikuwa nachukuliwa sana na hisia kipindi hicho kwa sababu wakati ule, mtu husika alikuwa hanipi majibu niliyokuwa nategemea kuyapata. Nikaona bora nijitoe ufahamu. Ila ni bora tu kuwa nuwazi na kusema nilikuwa na wivu na sikuwa najiamini“. <<< Chris Brown.
Kuhusu mwanae na jina la Album yake, Chris Brown alisema: >>> “Album inabeba vitu vingi maishani mwangu, kwanza inabeba uhalisia wa sehemu nilipo katika maisha yangu sasa hivi, Royalty amechukuwa nafasi kubwa maishani mwangu na najua siwezi kuwa mtu bora kwa wengine basi walau nijaribu kufanya vitu vizuri kwa ajili yake, mwanangu amenisaidia sana…” <<< Chris Brown.
Unaweza ukaicheki interview nzima ya Chris Brown na kipindi cha ‘Ebro In The Morning’ hapa chini kwenye hii video.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE kwa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE