Habari za Mastaa

Chris Brown alitaka haki zote juu ya mtoto pia, je kafanikiwa!? Mahakama imeamua haya…

on

Baada ya mgogoro mrefu kati ya Chris Brown na mama wa mtoto wake Nia Guzman sasa Mahakama ya Houston imetoa maamuzi na utaratibu wa jinsi ya kukaa na mtoto Royalty kwa wazazi hao wawili…

Nia Guzman alipeleka madai yake Mahakamani kuwa R&B staa Chris Brown sio baba mzuri kwa mtoto huyo na hivyo angependa kama Mahakama ingemruhusu kukaa na mtoto huyo moja kwa moja lakini sio na Chris.

chris and nia

Chris Brown na Nia Guzman.

Chris Brown aliyapinga kabisa madai hayo na kusema kuwa mwanamke huyo anamtumia mtoto wao kama kitega uchumi ili kuvuna pesa nyingi kutoka kwake na madai ya kuwa yeye sio baba mzuri kwa mtoto huyo ni moja tu ya njama zake kuhakikisha anapata pesa nyingi kutoka kwake.

cb-royalty3

Royalty na mama yake Nia Guzman

Sasa jana wawili hao walikua Mahakamani jijini Houston, wote wakiwa wanagombania kitu kimoja, haki zote za kukaa na mtoto… baada ya kukaa Mahakamani hapo kwa masaa mawili, Judge aliyekuwa anasikiliza kesi hiyo alipinga kuwapatia wazazi hao haki zote za kukaa na mtoto na kuamua  kuwa wawili wao watashirikiana kwa pamoja kukaa na mtoto huyo ( 50/50 physical custody).

cb-royalty4

Royalty.

Mahakama imeamua kuwa Royalty atakuwa anakaa na wazazi wake kwa zamu za siku nne kwa kila mmoja, yaani atakuwa anakaa kwa mama yake Nia Guzman kwa siku nne na kumalizia siku nyingine nne  kwa baba yake Chris Brown… haya ndio maamuzi ya mwisho ya Houston Courtroom juu ya ugomvi huo wa mtoto.

Kwa sasa wazazi wote wawili, Chris Brown mama yake Royalty, Nia Guzman wanakaa Los Angeles.

PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia za siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos

Soma na hizi

Tupia Comments