social network

Chris Brown na tattoo mpya kichwani, hii ndio maana yake…!

on

cbb

Siku chache zilizopita Chris Brown aliweka headlines kwenye Instagram na kwenye mitandao baada ya kuongeza tattoo mpya mwilini mwake… kilichotushangaza zaidi tattoo hiyo haijawekwa sehemu yoyote ile mwilini mwake bali kichwani kwake!

Kama wewe ni mfuatiliaji mzuri wa Chris Brown utakua unajua kua staa huyo wa muziki sio mgeni wa kujichora tattoo mwilini, ana tattoo nyingi mwilini mwake na tattoo yake ya kwanza aliipata akiwa na miaka 13!

tattcb

Tattoo mpya ya Chris Brown aliyoichora nyuma ya kichwa chake!

Tattoo hii mpya imeleta maneno mengi ya mshangao huku mashabiki wake wengi kwenye Instagram wakijiuliza staa huyo ana maanisha nini kujichora kichwani na wengine kuhisi labda pesa alizonazo zinamfanya awe chizi. Yote yalijibiwa baada ya Chris Brown kupost picha kwenye Instagram yake akieleza maana ya tattoo yake mpya.

tattcb

>>> “Venus De Milo: Malkia wa Upendo. Nyumbu; anawakilisha nyota ya Ng’ombe ambayo ni ya kwangu. Kwa makusudi kabisa imewekwa upande wa kushoto kichwani kwangu kwa ulinzi wa moyo wangu na kwa wa upendo wa Malkia wangu… ROYALTY ni kila kitu kwangu na kama mwanaume, nitamlinda kwa kila kitu”. <<< @chrisbrownofficial.

Licha ya hayo, Chris Brown aliweka wazi ili watu wamuelewe kwa kusema kuwa anaweza kufanya chochote anachokita!

Je  hii imekaaje na unaionaje mtu wangu!?

PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia za siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos

 

Soma na hizi

Tupia Comments