social network

Chris Brown awashambulia TMZ na kumsema mwanzilishi wake…!!

on

Wasanii wengi wa Marekani sio washabiki wakubwa wa website ya TMZ na mmoja ya wasanii hayo ni R&B Superstaa Chris Brown.

Chris Brown amekuwa akisikika sana akiwashambulia TMZ kwa taarifa wanazoziandika juu yake ambazo kwa asilimia kubwa amekuwa akizipinga… inaonekana time hii Chris Brown hajapendezwa tena na taarifa za TMZ na kuamua kumshambulia mwanzilishi wa site hiyo Harvey Levin kupitia page yake ya Instagram!

brown3

TMZ wanadai kuwa Chris aliivunja mkataba kati yao baada ya msanii huyo kutokutokea kwenye tamasha la Black Gay Pride Event jijini Atlanta siku ya tarehe 7 September mwaka huu…

Chris Brown amepinga taarifa hizi na kudai kuwa wala hakuambiwa au kufanyiwa booking yoyote ya tamasha hilo… pia amemshambulia mwanzilishi wa website hiyo Harvey Levin na kusema “kwasababu yeye ni shoga basi angekuwa anahangaika kutafuta njia za kuwasaidia mashoga wengine” na sio kuandika uongo juu yake!

brown2

Kupitia Instagram yake Chris alipost picha na ujumbe mrefu kuwasema TMZ

cb

>>> “Jamani TMZ ifike hatua muache kuandika mambo ya kijinga…sijawahi kuwekwa booking! Mnapenda sana kusema kuwa siwapendi mashoga ili kupata tu sababu ya kuniongelea… sijali kama wewe ni shoga Harvey… badala ya kuandika vitu unavyoviandika unatakiwa uwe unatafuta namna ya kuwasaidia watu kama wewe ambao wanaona aibu kusema wapo vile walivyo… hebu jaribu kurekebisha focus ya webite  yako…” <<< @chrisbrownofficial.

PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia za siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos

 

Soma na hizi

Tupia Comments