Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeridhia maombi ya mshitakiwa ambaye ni raia wa Burundi Ferdnand Ndikuriyo(27) maarufu ‘Chuma cha Chuma, ya kupewa dhama iwapo tu atatimiza masharti aliyopewa.
Uamuzu huo ulitolewa mahakamani hapo na Hakimu Mkazi Mkuu, Yusto Ruboroga shauri hilo lilipoitwa kwa ajili ya uamuzi wa mshitakiwa kuoata dhamana baada ya upande wa mashitaka kuwasilisha pingamizi zao.
Alisema ilikuwa ni kwa ajili ya uamuzi wa shauri la pili juu ya pingamizi la dhamana ambao liliwasilishwa na upande wa mashitaka.
Aidha, Ruboroga alisema kwa kawaida pingamizi huwa linawasilishwa ndani ya shauri linalomkabili mshitakiwa ktika mahakama husika lakini kwa hapo ilikuwa utofauti kwani ingamizi juu ya dhamana yake lili wasilisha chini ya maombi ambayo aliyasoma mahakamani hapo.
Alisema upande wa mashitaka ulidai mshitakiwa asipewe dhamana kwa kuzingatia kuwa alikuwa ni raia wa kigeni na hakuwa na hanuani halisi ambayo ilikuwa ikieleza kuwa mshitakiwa ni mkazi wa wapi hapa nchini.
Aliongeza kuwa kwa upnade wa utetezi walidai kuwa pingamizi hizo hazijakaa kisheria, hivyo ni maneno tu kama simulizi na kuiomba mahakama iyapuuze kwani walisema mshitakiwa anamahali pa kuishi ambapo anaishi na mke pamoja na mtoto wake.
Pia walidai hati ya kusafiria ya mteja wao ipo kwa maofisa wa uhamiaji na kuiomba mahakama itupilie mbali pingamizi hizo.
Alisema kwa kuzingatia hayo aliamua kuwa mshitakiwa anahaki ya kupewa dhamana iwapo tu atatimiza masharti aliyopewa ambayo yalikuwa ni mshitakiwa kusaini bondi ya Sh milioni 10 na kuwa na wadhamini wawili ambao ni watanzania waliotakiwa kusaini bondi ya Sh milioni 10.
Pia Ruboroga aliongeza kuwa atatakiwa kuweka benki Sh milioni 20 au kuwasilisha mahakamani hati ya mali isiyohamishika yenye thamani sawa na kiasi hicho.
Aliongeza kuwa mshitakiwa anatakiwa kuwasilisha hati na nyaraka zote za kusafiria mahakamani na pia alisema hatotakiwa kusafiri kwenda nje ya Mkoa wa Dar es salaam bila kuwa na kibali cha mahakama.
Baada ya kusema hayo hakimu aliahirisha kesi hiyo hadi leo kwa ajili ya kuendelea na kesi ya msingi, hivyo aliutaka upande wa mashitaka kama upelelezi umekamilika waweze kuendelea.
Mshitakiwa alirudishwa rumande kwani bado hakuweza kutimiza masharti ya dhamana.
Kwa mujibu wa hati ya mashitaka alidai Chuma alitenda kosa hilo Septemba 18,mwaka huu eneo la Upanga, Las Vegas Casino Wilaya ya Ilala Dar es Salaam. Ilidaiwa kuwa, mshitakiwa akiwa eneo hilo, alibainika kuwepo nchini bila kibali.