Chuo Cha ufundi stadi veta kihonda kimetoa Mafunzo ya ufundi hususani ya kilimo Kwa Wanafunzi 240 kutoka shule ya sekondari ya padri pio ambayo ipo jirani na chuo hicho.
Mkuu wa chuo Cha Veta Kihonda Theresa Mosha akizungumza na wahitimu wa chuo hicho amesema wameamua kuwachukua Wanafunzi hao na kuwapa stadi za maisha lengo likiwa ni kuimalisha ushirikiano, ujirani mwema pamoja na kuwasaidia vijana kujikwamua kiuchumi baada ya kuhiti.u elimu Yao sekondari.
Mkuu huyo wa chuo alisema kuwa vijana hao ambao wamewachukua na kuwapa elimu ya ufundi stadi Hasan kwenye kilimo Cha mbogamboga na mahindi, wamekuwa mstari wa mbele Katika kujifunza na kuelewa wanachokifanya na chenye manufaa kwao.
Kwa upande wake meneja rasilimali watu kutoka shirika la reli ya mwendokasi Tanzania SGR Elifadhiri Msuya amewataka wazazi na walezi kuwaruhusu watoto wa like kujiunga na vyuo vya ufundi stadi veta kwani hakuna kazi inayomshinda mtoto wa kike .
Aidha alisema kuwa Katika maeneo mengi tumeshuhudia kazi nyingi za ufundi zikifanywa na wanawake na kumekuwepo na fursa nyingi za ufundi Kwa watoto wa like.