Chuo Kikuu cha Ardhi na Kampuni ya Kichina ya Ujenzi ya Group Six International ikishirikiana na Chuo cha Chong Ching Vocational Institute of Engineering cha China imetekeleza makubaliano ya awali ya serikali ya Mji wa Chong Ching nchini China ya kujengwa kwa Karakana za kisasa katika Chuo Kikuu cha Ardhi na kwenye mradi wa Sino Tan wa ujenzi wa Viwanda katika Eneo la Kwala Satelite City mkoani Pwani,
Utiliaji Saini wa makubaliano hayo yalifanyika July 2022 katika ufungaji wa maonyesho ya kibiashara (Tanzania Trade Expo), ambapo mgeni rasmi alikuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Dk, Philip mpango, katika makubaliano hayo jumla ya wahandisi kutoka nchini Zaidi ya 100,000 watafaidika kupitia ujenzi wa Karakana hizo katika kujiongezea ujunzi na maarifa,
Aidha, katika makubaliano hayo yapo mambo kadhaa yalibainishwa na kupitishwa ikiwemo kutolewa kwa mafunzo ya kuwajengea uwezo wa ufanisi wa ujenzi katika miradi mikubwa inayotekelezwa hapa nchini hususani wahandisi watakaofanya kazi katika mradi mikubwa wa ujenzi wa viwanda uliopo Kwala Sino Park industrial,
Vilevile walikubaliana katika kubadilishana uzoefu kati ya wanafunzi na wahadhiri kutoka katika Chuo cha Chonq Ching Vocational Institute of Engineering na Chuo cha Kikuu cha Ardhi na Taasisi ya Teknolojia Dar es salaam ili kujiongezea ufanisini katika amali ya ujenzi.
Akizindua Karakana hiyo hivi karibuni Jijini Dar es Salaam Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia, Prof Adolf Mkenda alisema kuwa Karakana hizo zitakuwa mkombozi katika sekta ya Uhandisi na elimu ya Sanyansi na Teknolajia hapa nchini, kwani Wahandisi wengi Pamoja na wanafunzi wanaosomea masomo ya uhandisi wataweza kupata ujuzi unaotokana na kujifunza kwa vitendo zaidi kupita vifaa vilivyomo kwenye Karakana hizo.
“Lubani workshop ni (Karakana ya kisasa ya kufundishia kutoka China) imezinduliwa nchini na kuwa nchi ya 10 Barani Afrika ikiwa ni kutekeleza wazo la Rais wa Jamhuri ya Watu wa China, Xhi Jin Pin, la mwaka 2018 alilolitoa Jijini Beijing, la kuwa ongezea uwezo wataalamu wa Uhandisi Barani Afrika Ili kuendana na mabadiliko ya teknolojia na kuendana na soko la ajira lililopo katika Viwanda na Makampuni ya kachina yaliyopo katika nchi hizo”. Alisema Prof Mkenda.
Akizindua Karakana kama hiyo iliyopo katika eneo la ujenzi wa Viwanda mkoani Pwani katika eneo la Kwala Dk Godwin Maro ambaye ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Utafiti wa Majengo kutoka Chuo Kikuu cha Ardhi, akimwakilisha Makam Mkuu wa Chuo hicho, alisema kuwa ujenzi wa karakana hiyo ya kisasa ambayo itatoa fursa kwa wanafunzi na wahadhiri kada ya uhandisi kujifunza jinsi karakana hiyo invyofanya kazi pia kuna fursa ya wanafunzi kwenda nchini china kusoma na kujionea Teknolojia mpya ya ujenzi na kubadilishana ujuzi wa kazi.
Aidha, Dk, Maro alitoa rai kwa wanafunzi watakaopata mafunzo katika karakana hiyo kuwa wabunifu na makini sana kwani kupitia vifaa vilivyopo kwenye Karakana hiyo itawasaidia kuongeza wigo na uwelewa Zaidi katika majukumu yao mara wamalizapo masomo yao pamoja na wahandisi ambao watapata fursa ya kufanyia kazi katika mradi wa SinoTan industrial park itawajengea uwezo wa jinsi ya kuendesha mitambo mikubwa katika miradi ikiwemo wa majengo makubwa, barabara na madaraja .
“moja ya sababu ya kufungua karakana hapa nchini ni kuongeza mnyororo wa thamani na kuongeza fursa za ajira hapa nchini na wataalamu wengine kwenda kufanya kazi nje ya nchi” alisema Dk, Maro.
Vilevile, Dk Maro alisema kuwa Karakana hiyo itatumika katika mafunzo ya darasani kwa wanafunzi ambao mara nyingi Kampuni ya Ujenzi ya Group Six International inakuwa na utaratibu wa kufanya kazi na wanafunzi wa kada ya uhandisi na kuweza kuwaongezea uwezo kwa kupata mafunzo na kuweza kuona jinsi ya mabadiliko ya vitendea kazi vya kisasa vinavyofanya kazi.
Dk, Maro alisema kuwa uwepo wa Karakana hiyo pia itatarajia kuwa msaada mkubwa kwa wahandisi wanaochipukia ili kuweza kupata mafunzo hayo kwa kupata fursa ya kuleta maendeleo hapa nchini.
Aidha, Dk Maro alisema kuwa mafunzo hayo watakayopata katika karakana hiyo ya kisasa yataleta utandawazi katika sekta nzima ya ujenzi na kuleta mapinduzi katika taaluma nzima ya uhandisi na uchumi.
Naye, Mwenyekiti wa Sino Tan industrial Jensen Huen amewataka wahandisi na wanafunzi wote wanaosomea masomo ya uhandisi kutumia mafunzo watakayopata katika karakana hizo kwa kupata uzoefu katika taaluma hiyo ya ujenzi.
Jensen, alisema kuwa Karakana hiyo ni mpango endelevu na tangia ulipoanzishwa nchini china umekuewa ukifanya kazi kwa umakini kutokana uko umeleta majibu chanya kuanzia kwenye nchini china mpaka kwenye miradi.
Pia, italeta utengamano baina ya nchi ya China na zile za Afrika ambazo zimeingia mkataba wa mafunzo hayo hususani Tanzania watafaidia na mafunzo ya darasani na usimamizi wa miradi mikubwa.
“Kwa kuwa nchi hizi mbili zina mahusiano mazuri toka kipindi cha urafiki wa siku nyingi kati ya Mwalimu Julius Nyerere na Rais wa Kwanza wa Jamuhuri ya Watu wa China Mao TseTong na Serikali mji wa chonq ching ya China iko tayari kutoa ufadhili kwa walimu na wanafunzi wa kitanzania kwenda China kujifunza na walimu wa chuo cha chonq vocational institute of engineering kuja nchini kubadilishana uzoefu” alisema Jensen
Aidha, Jensen Huen alisema kuwa mbali na uzinduzi wa karakana hiyo pia kampuni ya group six international itaendelea kutoa nafasi kwa wanafunzi na wataalamu wa ujenzi kwenda nchini China ili waweze kujifunza jinsi ya mabadiliko ya teknolojia katika ujenzi inavyofanya kazi.
Mwenyekiti huyo, alisema kuwa Karakana hiyo ya kisasa imeasisiwa Nchini China na kuletwa Africa ili kusaidia wakandarasi wakongwe na wanaochipukia ili kuweza kupata uzoefu katika tasnia nzima ya uhandisi.
Tanzania nan nchi nyingine 14 za Africa zikiingia katika makubaliano ya ujenzi wa Karakana za kisasa ikiwemo Kenya, South Africa, Mali, Nigeria, Egypt, Uganda, Cote d’Ivoire, Madagascar, and Ethiopia.