Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Prof Adolf Mkenda amebainisha kuwa dhumuni ya serikali ya Awamu ya Sita kutoa ni kuweka kipaumbele katika sekta ya Ujenzi, kwa kuanzishwa program maalumu za kuwajengea uwezo Wahandisi na wakadiliaji Majengo ili kupata wataalamu wa kutosha watakaosaidia kuleta ufanisi wakati wa utekelezaji wa miradi inayotolewa na serikali.
Profesa Mkenda ameyasema hayo hivi karibuni Jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa Karakana ya kisasa iliyojengwa katika Chuo Kikuu cha Ardhi na Chuo cha chonq ching vocational institute of engineering cha nchini China kwa uratibu wa kampuni ya ujenzi ya group six international.
Aidha, Prof Mkenda alisema kuwa Karakana hiyo itakuwa ya 10, kujengwa katika nchi za Africa tangu mradi wa Lubani uanzishwe mwaka 2019, baada ya azimio kupitishwa katika mkutano baina ya China kwa kushirikiana na nchi za Africa uliofanyika mwaka 2018 ambao unalenga kuleta maendeleo katika sekta ya Uhandisi ambazo nchi hizo zitafaidika na mafunzo ya kuwajengea uwezo kwa Wakandarasi wakongwe na wanaochipukia.
“Karakana hiyo itatumika katika mafunzo ya darasani kwa Wahadhiri hao wa Chuo Kikuu hicho cha Ardhi Kitivo cha Uhandisi wa Majengo na kuweza kuwaongezea uwezo Wahadhiri hao, kwa kupata mafunzo na kuweza kuona jinsi ya mabadiliko ya vitendea kazi vya kisasa vinavyofanya kazi”. Alisema Prof Mkenda.
Kwa upande wake Makamu wa Chuo cha Ardhi Prof Evarist Riwa alisema kuwa Karakana hiyo itakuwa kitovu ch mafunzo ya Uhandisi na yataleta ufanisi mkubwa kwa wataalamu hao na kuwapa wigo mkubwa kwa kujua mabadiliko ya teknolojia pamoja na kujua jinsi ya kufanya kazi kwa usalama na uendeshaji wa miradi mikubwa kwa kutofautisha ukandarasi wa ujasiriamali na kuwa ukandarasi wenye tija na kuleta maendeleo katika sekta ya uhandisi.
Prof, Riwa alisema kuwa uwepo wa Karakana hiyo pia itataraji kuwa msaada mkubwa kwa wahandisi wanaochipukia ili kuweza kupata mafunzo hayo kwa kupata fursa ya kuleta maendeleo hapa nchini.
Kwa upande wake balozi wa china nchini Tanzania Bi Chen Ming Jiang amekitaka Chuo Kikuu cha Ardhi pamoja na wanafunzi wote wanaosomea masoma ya uhandisi kutumia mafunzo hayo na kupata uzoefu katika taaluma hiyo ya ujenzi.
Balozi huyo alisema kuwa Karakana hiyo ni mpango endelevu na tangia ulipoanzishwa nchini china umekuewa ukifanya kazi kwa umakini kutokana uko umeleta majibu chanya kuanzia kwenye nchini china mpaka kwenye miradi
Naye makamu mwenyekiti wa makampuni wa group six international Jensen Huen amesema kuwa mbali na uzinduzi wa karakana hiyo pia kampuni ya group six international itaendelea kutoa nafasi kwa wanafunzi na wataalamu wa ujenzi kwenda nchini China ili waweze kujifunza jinsi ya mabadiliko ya teknolojia katika ujenzi inavyofanya kazi.
Amesema kuwa karakana hiyo ya kisasa imeasisiwa Nchini China na kuletwa Africa ili kusaidia wakandarasi wakongwe na wanaochipukia ili kuweza kupata uzoefu katika tasnia nzima ya uhandisi.